Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini,Dk. Charles Msonde akizungumza na wanahabari jijini Dar leo Februari 14,2015. Shule za sekondari za binafsi zaongoza 10 bora matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana 2014.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini (NECTA), Dk.Charles Msonde amesema katika matokeo ya kidato cha nne ya mtihani wa mwaka jana 2014 ufaulu umeongezeka kwa asilimia 12.67 ikilinganishwa na mwaka 2013.

Katika matokeo hayo msichana wa shule ya sekondari ya Baobab, Nyakaho I. Marungu ndio aliyeongoza mtihani huo na kufatia wavulana.

Shule za Sekondari za St.Fransis ya mkoani Mbeya wanafunzi sita na Feza wanafunzi nane na kufanya shule hizo kuingia katika 10 bora kwa kutoa idadi wanafunzi wengi ikilinganishwa na shule zingine.

Msonde amasema matokeo hayo yanatokana na mfumo mpya wa GPA kwa kuangalia masomo saba hivyo ufaulu umetokana na mfumo huo.

BOFYA LINK HII KUONA NA KUSOMA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE NA QT 2014 .


Aidha Jumla ya Watahiniwa 196,805 sawa na 68.33% ya watahiniwa wote waliofanya mtihani kidato cha IV mwaka 2014 wamefaulu ikiwa ni ongezeko la 10.08% kulinganisha na mwaka 2013 ambapo wanafunzi 235,227 sawa na 58.25 walifualu.

Akitangaza matokeo ya Kidato cha Nne ya mwaka 2014 leo Februari14,2015 jijini Dar es salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Dkt Charles Msonde amesema kati ya waliofaulu, wasichana ni 89,845 sawa na asilimia 66.61 wakati wavulana ni 106,960.

Amesema watahiniwa wa shule waliofaulu ni 167,643 sawa na asilimia 69.76 ya waliofanya mtihani, wasichana wakiwa 75,950 sawa na asilimia 68.70 na wavulana 91,693 sawa na asilimia 70.67.

Amesema mwaka 2013 watahiniwa 201,152 sawa na asilimia 57.09 ya watahiniwa wa shule walifaulu mtihani huo hivyo ufaulu kwa wanafunzi wa shule umepanda kwa asilimia 12.67 mwaka 2014 ikilinganishwa na mwaka 2013.

Akizungumzia ubora wa ufaulu, Dkt Msonde amesema kuwa jumla ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa madaraja ya Distinction, Merit na Credit ni 73,832 sawa na asilimia 30.72 wakiwemo wasichana 27,991 sawa na asilimia 25.32 na wavulana ni 45,841 sawa na asilimia 35.33.

Watahiniwa waliopata daraja la PASS 93,811 sawa na asilimia 39.04 na waliofeli kwa kupata daraja la FAIL 72,667 sawa na asilimia 30.24.

Kuhusu ufaulu wa masomo, Dkt Msonde amesema kuwa ufaulu katika masomo ya msingi umepanda kwa kati ya asilimia 1.28 na 11.22 ikilinganishwa na mwaka 2013.

Ufaulu wa juu kabisa umekuwa katika somo la Kiswahili ambapo asilimia 69.66 ya watahiniwa wote wamefaulu na ufaulu chini kabisa ni wa somo la Basic Mathematics ambapo asilimia 19.58.

Amesema Baraza limefuta matokeo ya watahiniwa 184 baada ya kubainika kufanya udanganyifu, kati yao 128 ni watahiniwa wa kujitegemea na 56 ni watahiniwa wa shule.

Akizitaja SHULE 10 BORA KWA UFAULU NI , Dkt Msonde amesema shule hizo nipamoja na :-

Kaizirege mkoa wa Kagera

Mwanza Alliance mkoa wa Mwanza

Marian Boys mkoa wa Pwani

St. Francis Girls mkoa wa Mbeya

Abbey mkoa wa Mtwara

Feza Girls mkoa wa Dar es salaam

Bethel sabs Girls mkoa wa Iringa

Marian Girls mkoa wa Pwani

Feza Boys mkoa wa Dar es laam.

SHULE 10 ZA MWISHO NI PAMOJA NA:-

Manolo mkoa wa Tanga

Chokocho mkoa wa Pemba

Kwalugulu mkoa wa Tanga

Relini mkoa wa Dar es salaam

Mashindei mkoa wa Tanga

Njelekela Islamic Seminary mkoa wa Kigoma

Vudee mkoa wa Kilimanjaro

Mnazi mkoa wa Tanga

Ruhembe mkoa wa Morogoro

Magoma mkoa wa Tanga.

Dkt Msonde pia ametaja watahiniwa 10 waliofanya vizuri kuwa ni:-

Nyakaho Marungu kutoka Baobab Pwani

Elton Sadock Jacob kutoka Feza Boys Dar es salaam

Samwel M Adam kutoka Marian Boys Pwani

Fainess John Mwakisimba kutoka kutoka St Francis Girls Mbeya

Mugisha Reynold Lukambuzi kutoka Bendel Memorial Kilimanjaro

Paul W Jijimya kutoka Marian Boys Pwani

Angel Lundgreen Mcharo kutoka St Francis Girls Mbeya

Atuganile Cairo Jimmy kutoka Canossa

Jenifa Lundgreen Mcharo kutoka St Francis Girls Mbeya

Mahmoud Dadi Bakili kutoka Feza Boys.

KUANGALIA MATOKEO BONYEZA HAPA >>>>> MATOKEO KIDATO CHA NNE 2014.
 
 
 
Top