PICHA NA YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA UMOJA WA WANANGARA WAISHIO DAR ES SALAAM.
Kikao hicho kimefanyika siku ya Jumamsoi tarehe 30/08/2014 katika ukumbi wa AVIATION PARK Maeneo ya Banana Ukonga. Kikao hicho kimeanza kwa agenda ya kuchagua viongozi wataoongoza umoja huo. viongozi waliochaguliwa ni kama ifuatavyo:-
ELDAFONCE MAMBAMBA-MWENYEKITI
JOHN MESHAKI RUDAHEZA-MWENYEKITI MSAIDIZI
ASHERY MAJANJA-KATIBU
BWABA BAKILANE- KATIBU MSAIDIZI
GODFREY KITANGA-MHASIBU
JULIETH BANIGWA-MHASIBU MSAIDIZI
Aidha wanangara waishio Dar Es Salaam wamepanga malengo na mikakakti ya kudumisha umoja huo ikiwa ni pamoja na kuanzisha katiba ya umoja huo, kusaidiana na kuinuana kimitaji, kushiriki katika maendeleo ya wilaya ya Ngara ikiwa ni kuiendeleza Ngara na kusaidia wasiojiweza na watoto yatima, kuwawezesha wasomi wa Ngara kupata fursa ajira na kupanga mkakati wa kufungua ofisi ya umoja huo Dar Es salaam na Ngara.