CHAMA cha Wananchi CUF kimetoa msimamo wake wa kutoshiriki katika uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliotangazwa kufanyika Machi 20 mwaka huu kufuatia kusitishwa kwa zoezi la kutangaza matokeo ya uchaguzi uliofanyika October 20 mwaka 2015 kutokana na kubainika kuwepo na kasoro kadhaa.
Uamuzi wa CUF umetolewa January 28 Jijini Dar Es Salaam huku pia chama hicho kikiwataka wanachama wa chama hicho Visiwani Zanzibar kutoshiriki katika uchaguzi huo.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar Es Salaam Katibu Mkuu wa chama hicho na aliyekuwa Mgombea wa Urais wa CUF Visiwani Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ametoa msimamo wa chake kutokuhiriki katika uchaguzi huo kwa madai ya kutambua uchuguzi uliofanyika Oktoba 25 kwakuwa haukuwa na kasoro yoyote licha ya mwenyekiti wa tume ya uchuguzi wa Zanzibar Jecha Salimu Jecha kutilia mbali uchaguzi huo kwa madai ya kasoro mbalimbali zilizojitokeza wakati wa uchaguzi.

Nae Mwenyekiti wa kamati ya uongozi wa uongozi Taifa wa Chama hicho Bw.Twaha Taslima amesema chama hicho kinayatambua matokeo ya awali ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka 2015.

Bw.Taslima amesema hakuna kifungu chochote cha katiba au sheria ya Zanzibar kinachompa uwezo Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar kufuta au kuitisha uchaguzi wa marudio.

October 25 mwaka 2015 ni siku ambayo Tanzania ilifanya uchaguzi mkuu wa Rais,wabunge,wawakilishi na Madiwani,kwa upande wa Zanzibar kulikuwa na kasoro kadhaa zilizosababisha Tume ya uchaguzi Zanzibar ZEC kusitisha kutangaza matokeo,kufuatia hatua hiyo tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi Zanzibar imetangazwa kuwa ni march 20 2016.

Vyama ambavyo mpaka sasa vimetangaza kutoshiriki katika uchaguzi huo ni CUF, CHAUMA pamoja na vile visivyokuwa na wawakilishi Bungeni.












 
Top