Serikali imetoa ufafanunuzi kwa nini imekuwa ikizuia wakulima kuuza mazoa yao nje ya nchi kutokana na baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakiwalangua wakulima kwa kununua mazao hayo kwa bei ndogo tofauti na bei elekezi iliyotolewa na wizara ya kilimo chakula na ushirika.
Naibu waziri wa fedha na uchumi Mh Adamu Malima ametoa ufafanuzi huo Leo bungeni wakati akijibu swali la mbunge wa Rombo Mh Josephu Selasini aliyetaka kujua kwa nini serikali imekuwa ikizua wakulima kuuza mahindi nje ya nchi ambapo wafanyabiashara wangi wamekuwa wakija nchini kununa mahindi wengi wao wakitokea nchi jirani ya Kenya.
Mh Malima amesema kwa sasa serikali itaendelea kuzuia mahindi kuuzwa nje ya nchi huku wizara ya kilimo chakula na ushirika ikitakiwa kutoa bei elekezi haraka ili kuwalinda wakulima na walanguzi ambao wamekuwa wakiwanyonya wakulima kwa kununua bei ndogo na wao kwenda kuuza bei ya juu na kunufaika zaidi ya mkulima.