Muonekano wa Mwili wa Marehemu kwa nje |
Imeelezwa kuwa Merehemu Rebeka ambaye alikuwa akiishi kwa mwanae mkubwa Stanley Sengasenga katika mtaa huo alifika kwa Bundala muda huo baada ya kuitwa na Magreth Richard ambaye ni mke wa Bundala kwa ajili ya shughuli hiyo.
Jinsi Bi Rebeka alivyopigwa shoka kichwani hadi ubongo kutoka nje |
Katika maelezo yake Magreth amesema Mama mkwe wake Marehemu Rebeka alifikia sebuleni, na kwamba wakati yeye yuko nje, alimwona mtu ambaye hakuweza kumfahamu akitoka sebuleni hapo na kukimbia ndipo alipoangalia na kumkuta Rebeka ameuawa.
Taarifa za awali zimedai, kabla ya tukio Magreth ambaye kwa sasa anashikiliwa na jeshi la polisi mjini Kahama kwa mahojiano alienda nyumba ya jirani kuazima Shoka, ambalo baadaye limekutwa kwenye shimo la maji taka nyumbani hapo.
Shoka hilo limepatikana baada ya mbinu za kiupelelezi za Jeshi la Polisi kuagiza gari la maji taka kuyavuta maji hayo baada ya majirani kudai hawajaona mtu aliyekimbia na shoka muda huo katika mwelekeo ambao Magreth ameelekeza.
Jeshi la Polisi wilaya ya Kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Wilaya ya Kahama, huku upelelezi ukiendelea. Taarifa za awali zimedai, kabla ya tukio Magreth ambaye kwa sasa anashikiliwa na jeshi la polisi mjini Kahama kwa mahojiano alienda nyumba ya jirani kuazima Shoka, ambalo baadaye limekutwa kwenye shimo la maji taka nyumbani hapo.
Shoka hilo limepatikana baada ya mbinu za kiupelelezi za Jeshi la Polisi kuagiza gari la maji taka kuyavuta maji hayo baada ya majirani kudai hawajaona mtu aliyekimbia na shoka muda huo katika mwelekeo ambao Magreth ameelekeza.
Mwili wa Marehemu Bi Rebeka ukiondolewa eneo la tukio kupelekwa Mochwari chanzo:KAHAMA FM |