MICHEZO:- CHUO KIKUU CHA MWENGE(MWUCE) KILICHOPO MOSHI KILIMANJARO KIMESHINDA MECHI ZOTE ZA MPIRA WA MIGUU NA MPIRA WA WAVU DHIDI YA TIMU ZA CHUO KIKUU CHA MT. MERU KUTOKA ARUSHA
Chuo hicho kimepata ushindi huo katika uwanja wake wa nyumbani leo tarehe 19/6/2014 ambapo wageni hao kutoka Arusha wametembelea chuo hicho kwa ziara ya kimichezo kama ishara ya kudumisha undugu na upendo baina ya vyuo vikuu vya kanda ya kaskazini.
Katika ziara hiyo chuo cha Mount Meru kimeleta timu mbili, timu ya mpira wa miguu (football) na timu ya mpira wa wavu (volleyball) ila bahati haikuwa yao baada ya timu za mwenge kushinda michezo yote miwili.
katika mpira wa miguu chuo cha Mwenge kimeshinda gori 2 kupitia kwa washambuliaji wake Hamisi Kisu na Tumaini huku wageni hao wakiambulia sufuri (0).
Akiongelea mchezo huo kocha wa timu ya mwenge bwana Jacob amewasihi vijana kucheza kwa kujituma na kuheshimu maamuzi ya kocha atakayeshika nafasi yake maana yeye na wachezaji wengine akina Ezra Essau, Felix Dabana, Gaudin Gratian, Yahaya Kiliwasha, Rashid Yusuph, Martin, Elisha Mkilya na Michael wanamaliza muda wao wa kutumikia timu hiyo kwa sababu kipindi chao cha kuwepo Mwenge kama wanafunzi kimekwisha. Zaidi amewasihi kuendeleza ushindi waliopata leo na kuendelea kuweka rekodi ya kutofungwa uwanja wa nyumbani maana mechi hiyo ilikuwa ya kuwapima uwezo vijana wa mwaka wa kwanza na wa pili hivyo vijana wa mwaka wa tatu walikuwa nje kuwashangilia wenzao.
Pia katika mchezo wa mpira wa wavu, timu ya chuo cha Mount Meru haikuwa na bahati baada ya kulazwa seti tatu kwa mbili na timu ya chuo kikuu cha Mwenge.
Akiongelea ushindi huo kocha wa volley wa timu ya mwenge bwana Odindo amesema kuwa ushindi huo ni kutokana na mazoezi yanayofanya na timu hiyo, hivyo amewasihi wachezaji kuweka bidiii zaidi kwenye mazoezi ili kujiandaa na mechi mbalimbali.