MICHEZO:- Hatimaye FIFA yamuadhibu Suarez kwa kosa la kumng'ata beki wa Italy Giorgio Chiellini
FIFA imempatia adhabu mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uruguay na club ya Liverpool Luis Suarez ya kutocheza mpira wala kujihusisha na shughuli za mpira kwa muda wa miezi minne (4) na pia kutoshiriki mechi 9 za michezo ya kimataifa.
Raisi wa chama cha mpira wa Uruguay Wilmar Valdez amesema chama hicho kitaomba rufaa juu ya adhabu hiyo iliyomkumba Suarez. kama rufaa haitafanikiwa Suarez hata shiriki tena michuano hiyo ya kombe la dunia inayoendelea ncchini Brazil kutokana na kosa hilo la kumng'ata beki wa Italia Giorgio Chiellini siku ya mechi uruguay iliyoshinda gori moja kwa bila na kuifanya timu ya Italia kuaga mashindano hayo.
Kama rufaa haitafanikiwa Suarez hatachezea club yake mpaka tarehe 26 Octoba, hali itakayomfanya kutoshiriki mechi 9 za ligi ya uingeleza na mechi 3 za kombe la vilabu vya ulaya (UEFA champion league) akiwa na Liverpool. FIFA imesema adhabu hiyo haitazuia uhamisho wake endapo Liverpool itaamua kumuuza kwa klabu nyingine, ikumbukwe mshambuliaji huyo alikuwa anawindwa na klabu ya mbili za Hispania, klabu ya Barcelona na Real Madrid.