Serikali ya CHINA imekabidhi msaada wa gari la kisasa la kurushia matangazo ya nje ya televisheni kwa Shirika la Utangazaji TANZANIA, TBC, lenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni SITA.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa gari hilo jijini DSM, Makamu wa Rais wa CHINA, LI YUCHUAN amesema msaada huo unalenga kudumisha uhusiano mwema kati ya nchi hizo mbili na kuongeza kuwa serikali yake inaamini kuwa utatumika kuwaunganisha Wachina na Watanzania kupitia vipindi mbalimbali katika Nyanja za Uchumi, Elimu, Sayansi, Teknolojia na Utamaduni.
 
Top