Mchezo huo wa burudani umechezwa leo tarehe 21/06/2014 katika uwanja wa chuo kikuu cha Mwenge ikiwa ni sehemu ya kutoa burudani kwa mashabiki na kuikaribisha serikali mpya madarakani.
Timu hizo zimeongozwa na Maraisi wote wawili ambapo ile ya wastaafu imeongozwa na Raisi mstaafu bwana Gaudin Gratian na ile iliyopo madarakani imeongozwa na Raisi Philipo Mwanga. Katika mchezo huo wa burudani kwa mashabiki timu ya wastaafu imeshinda jumla ya gori 5 kwa 0 magori yakifungwa na Ezra Essau waziri mstaafu wa starehe na burudani( social affairs) akitupia magori 4 na gori la tano likiwekwa nyavuni na beki wa kushoto Boniventure Mkulu aliyekuwa waziri mkuu wa serikali hiyo kupitia mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa seriakali mpya kunawa mpira kwenye eneo la hatari.

Mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa matokeo yalikuwa gori 5 kwa 0.
 
Top