AJALI:-Mbunge wa Tabora Aden Rage apata Ajali njiani kuelekea Dodoma.
Mbunge wa Tabora Mjini (CCM) Ismail Aden Rage, ambaye pia ni mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, akiwa amelazwa kwenye hospitali ya Rufaa, Dodoma, Jumatatu Agosti 4, 2014. Rage alipata ajali eneo la Chigongwe, nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma, wakati akielekea mjini humo tayari kushiriki vikao vya Bunge Maalum vinavyoanza Jumanne Agosti 5, 2014.
MBUNGE wa Tabora mjini (CCM), Ismail Aden Rage (pichani) na wenzake wanne wamenusurika kifo baada ya kupata ajali na gari lao walilokuwa wakisafiria kutoka Tabaora kwenda Dodoma eneo la Chigongwe mkoani Dodoma leo(Agost 04,2014).
Ajali hiyo imetokea baada ya dereva wa gari walilokuwemo kujaribu kulikwepa lori lililokuwa mbele yao na kupinduka.
Rage alikuwa anaelekea mkoani Dodoma kwa ajili ya vikao vya Bunge Maalum la Katiba vinavyoanza kesho.
Mbunge wa Sikonge mkoani Tabora kupitia CCM, ambaye pia ni Mujumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Said Nkumba, akimjulia hali Rage, hospitalini mjini Dodoma, Jumatatu Agosti 4, 2014.