Jeshi la Nigeria limedaiwa kutenda uhalifu wa kivita
Shirika la Amnesty International linasema kuwa limepata ushahidi wa uhalifu wa kivita Kaskazini mashariki mwa Nigeria, ambapo wanajeshi wanakabiliana na kundi la wapiganaji wa kiislamu- Boko Haram.
Pande zote mbili zinalaumiwa kwa makosa hayo.

Serikali ya Nigeria inasema kuwa unyama huo hauna nafasi katika jeshi huku ikiahidi kufanya uchunguzi.Katika video moja ya kuogofya, watu waliodaiwa kuwa wanajeshi wa Nigeria na wapiganaji wanaoungwa mkono na serikali, waliwachinja kinyama wafungwa waliokuwa wamewazuilia.

Boko Haram pia linalaumiwa kwa kufanya unyama mkubwa dhidi ya binadamu.

Amnesty inalaumu tume huru ya uchunguzi katika kile inachokiita misururu ya ukiukaji wa haki za kibinadamu kutoka kwa pande zote mbili.
 
Top