AUAWA KWA KUCHOMWA CHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI MAKABURINI
Mtu mmoja ambaye hajatambulika amekutwa ameuawa kwa kuchomwa chomwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kitu chenye incha kali katika makaburi ya misuna Singida mjini.
Wakielezea tukio hilo balozi wa mtaa wa mwenge Bi. Mary Mwambusu na mwenyekiti wa mtaa wa misuna Bwana Sarota Masawe wamesema tukio hilo linaonekana kutokea majira ya alfajiri ya siku ya tarehe tano mwezi wa nane katika makaburi ya misuna.
Viongozi hao wa mtaa Mwenge na Misuna wamesema tukio hilo ni la kwanza kutokea lakini wameliomba jeshi la polisi kuimarisha ulinzi hasa maeneo kama hayo ilikudhibiti mauaji kama hayo yasi tokee tena.
Akiongea kwa njia ya simu kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida Bwana Geofrey Kamwela amethibitisha kutokea kwa tukio hilo katika eneo la makaburi yaliyopo misuna Singida mjini na amesema jeshi lake bado linaendelea na uchunguzi kuweza kubaini chanzo cha mauaji hayo ambayo ni ya kinyama.