Wapiganaji wa Boko haram
Watu wanaodaiwa kuwa ni kundi la Boko Haramu wameshambulia raia na wanajeshi kaskazini mwa Cameroon ambapo watu kumi wanasadikiwa kufariki dunia.

Shambulio hilo linakuja baada ya shambulio jingine la hivi karibu ambapo wapiganaji wa kundi hilo walivuka mpaka kutoka Nigeria na kufanya mashambulizi kadhaa kwa wiki za hivi karibuni nchini Cameroon.
Tayari majeshi kutoka katika ukanda huo yameahidi kupambana na wapiganaji hao wa Boko Haramu walioua watu 4000 wasio na hatia kwa mwaka huu pekee.

Ni shambulizi la mchana la kusikitisha. Waendesha piki piki wanadaiwa kuwa ni wapiganaji wa Boko Haram waliolenga kukishambulia kijiji caha Zigague kaskazini mwa Cameron.

Walimshambulia kiongozi wa jadi wa baadae kurushiana risasi na kundi la wanajeshi wa Jeshi la Cameroon. Mwanajeshi mmoja aliuawa pamona na raia nane.

Kundi hilo pia lilishambulia kituo cha polis.

Katika siku za hivi karibu wapiganaji wa Boko Haramu wamekuwa wakifanya mashambulizi katika nchi ya Cameroon. Kumekuwa na matukio kadhaa ya utekaji nyara jambo lilosukuma jeshi kuanza mapambano ya angani.

Mashambulizi mengi yanayofanywa Boko Haramu yamekuwa yakielekezwa nchini Nigeria ambapo mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema zaidi ya watu 4000 wameuawa kwa mwaka huu pekee.

Karika siku za hivi karibuni, Camerooni, Nigeria, Chad na Niger zilikubalina kuunda jeshi la pamoja la kanda hiyo ili kupambana na wapiganaji hao wa Boko Haramu. Hata hivyo Cameoroon wakati inatafuta namna ya kupambana Boko haram kunaongeza hali isiyo tabirika ya kuongezeka kwa mashambulizi.
 
Top