Mabingwa wa Ligi kuu England msimu wa 2013/2014, Manchester City, Leo Agosti 30,2014,wamechapwa kwa Uwanja wa Etihad Bao 1-0.Bao la ushindi la Stoke limefungwa na Mchezaji wa zamani wa Man United, Mame Biram Diouf, katika Dakika ya 28 baada ya kukokota Mpira Mita 70 na kumzidi akili Kipa Joe Hart.

Huo ulikuwa ushindi wa kwanza wa Stoke dhidi ya City katika Mechi 12 za Ligi Kuu England Uwanjani Etihad na umekuja chini ya Meneja Mark Hughes ambae ni Mchezaji wa zamani wa Man United na pia Meneja wa zamani wa City.




Nae Kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson (mbeke) akiwa na David Gill na Sir Bobby Charlton wakitazama mchezo wa timu hiyo leo Agosti 30,2014,ikilazimishwa sare ya 0-0 na Burnley.


Man United imekuwa ikisuasua tangu kustaafu kwa Ferguson mwaka jana. Makocha wawili wamekwishapewa timu, David Moyes aliyetimuliwa mwishoni mwa msimu uliopita 2013/2014 na Ryan Giggs akakaimu kumalizia msimu, kabla ya msimu huu kuajiriwa Louis Van Gaal ambaye leo amefikisha mechi ya tatu bila ushindi, sare mbili ugenini, nyingine 1-1 na Sunderland na kufungwa moja nyumbani na Swansea City 2-1.



Magoli 2 ndani ya Dakika 3 za kwanza ziliwapa Chelsea mwanzo mzuri Ugenini huko Goodison na Chelsea wakamaliza Mechi hii kwa ushindi wa Bao 6-3.


Bao hizo za mapema za Chelsea, zenye utata wa Ofsaidi, zilifungwa na Diego Costa na Ivanovic.


Everton walipata Bao lao la kwanza katika Dakia ya 45 kupitia Mirallas.
Hadi Mapumziko Chelsea 2 Everton 1.


Kipindi cha Pili, Chelsea walipiga Bao la 3 mfungaji akiwa Coleman, alirjifunga mwenyewe, na Naismith kuipa Everton Dakika 2 baadae lakini Chelsea wakapiga Bao la Nne kupitia Matic na Dakika 2 baadae Mchezaji mpya wa Everton, Samuel Eto’o akaipigia Everton Bao la 3.


Huku Gemu ikiwa 4-3, Ramires akaipa Chelsea Bao la 5 katika Dakika ya 76 na Diego Costa akapiga Bao la 6 kuikata maini Everton.




Everton 3.


-Mirallas 45
-Naismith 69
-Eto'o 76


Chelsea 6.


-Diego Costa 1 & 90
-Ivanovic 3
-Coleman 67 [Kajifunga mwenyewe]
-Matic 74
-Ramires 77


Kesho Jumapili zipo Mechi mbili za Ligi Kuu England kati ya Aston Villa na Hull City na kufuatia ile ya Leicester v Arsenal


As It Stands Table EPL 2014/2015.


PositionTeamPlayedGoal DifferencePoints
Moving up 1Chelsea379
Moving up 2Swansea359
Moving down 3Tottenham256
Moving down 4Man City336
No movement 5Arsenal214
Moving up 6Southampton314
Moving down 7Hull214
Moving down 8Aston Villa214
Moving up 9Stoke304
Moving down 10West Ham3-13
Moving down 11Liverpool2-13
Moving up 12QPR3-43
Moving down 13Sunderland3-12
Moving down 14Man Utd3-12
Moving up 15Newcastle3-22
Moving down 16Everton3-32
Moving down 17West Brom3-32
Moving down 18Leicester2-21
Moving down 19Crystal Palace3-31
Moving down 20Burnley3-31



 
Top