Timu ya Kabanga fc
Mchezo huo umechezwa leo terehe 24/08/2014 katika uwanja wa Kabanga Ngara baada ya kuandaliwa na vijana wa timu hiyo wapenda michezo Ezra Essau na Deus Kaniki (mdhamini wa mchezo huo) kwa kushirikiana na viongozi wao. Hii ni baada ya kuonekana kuwa mpira kwa kata ya Kabanga umesahaurika tofauti na siku za nyuma, hivyo lengo la mchezo huo ilikuwa ni kuinua hamasa ili siku zijazo vijana wajitokeze kwa wingi mazoezini.
Timu ya Muyinga star
Mchezo huo ulokuwa wa kuvutia umechezwa katika uwanja huo wa Kabanga ambapo timu rafiki kutoka Muyinga Burundi wameibuka na Ushindi wa gori 4 ka 2 dhidi ya wenyeji Kabanga. wachezaji wa kabanga fc wamekiri kufungwa sababu ya kutokuwa na mazoezi na maandalizi ya kutosha na hii ni sababu ya wachezaji wengi kutokuhudhuria mazoezini.Aidha huo umekuwa mwanzo hivyo timu hiyo imejiandaa kuanza kujifua kimazoezi na kucheza mechi mbalimbali ili kuinua hamasa kwa vijana wa kabanga kupenda mpira kama zamani.
Timu ya Muyinga star ikinyosha misuli kabla ya mechi



