Mkurugenzi wa Wilaya ya Ngara alipokuwa akikabidhi mradi wa maji wananchi wa kijiji cha Ngundusi kata ya kabanga baada ya kukabidhiwa na mkandarasi wa mradi huo SIWASA ukiwa umekamilika tayari kwa matumizi.
Aidha akiongelea mradi huo diwani wa kata ya Kabanga Ndugu Said Soud alikili kupokea mradi huo ambapo alisema mradi huo ulifanikiwa kutokana na nguvu za wananchi pia na msaada kutoka benki ya dunia. wananchi walichangia sh. 3600000/= katika mradi huo ambapo benki ya dunia iliwaongezea shilingi 347,559,400 hivyo kukamilisha mradi huo.
Pia diwani huyo aliwasihi wananchi wa kijiji cha Ngundusi kuutunza mradi huo vizuri maana ni wa kwao ili uwe na faida kwa kizazi cha sasa na kijacho katika kijiji cha Ngundusi lakini kwa sasa mradi huo umegeuka kilio kwao.
Aidha wananchi wa kijiji hicho wamesema maji hayo yaliwahi kutoka mara tatu tu kwa baadhi ya maeneo na wakati maeneo mengine ya kijiji hicho bomba hazitoi maji kabisa tangu mradi huo umezinduliwa. wakazi wa kitongoji cha mkitamo kijiji cha Ngundusi wao wamesema maji huwa yanatoka mara moja moja jambo wanalohisi ni mgao. wananchi wamesema hakuna tofauti na kipindi cha nyuma kabla ya mradi huo maana kama ni shida ya maji bado iko palepale na kilio chao kikubwa ni kwa nguvu zilizotumika kuchimba mitalo na mchango wa kila kaya wa shilingi elfu tano ambao umeonekana kupotea bure.
Pia kwa upande wa wazee wasio jiweza ilikuwa kwamba watahudumiwa dumu mbili za maji bure na kwa kuzingatia afya zao yaani kuhudumiwa haraka wafikapo bombani lakini hali imekuwa tofauti maana wanadai hawapati huduma hiyo na zaidi wamesema pale maji yanapotoka japo ni kidogo hawapatiwi huduma hiyo kama ilivyopangwa zaidi hushinda kwenye foleni hadi maji kukatika bila kupata huduma.
Pia wananchi wamesema awali maji yalikuwa yanauzwa kwa shilingi 50 kwa dumu lakini bei imepanda hadi shilingi mia kwa dumu na cha kushangaza zaidi kwa sasa huduma hiyo ya maji haipatikani. Pia wananchi wanasema viongozi husika wanasema kuwa tatizo hilo limesababishwa na kupasuka kwa mabomba yanayosafirisha maji kutoka kwenye chanzo hadi kijijini huku wakisema kuwa nguvu ya mashini inayosukuma maji ni kubwa kuliko uwezo wa bomba hizo.
Pia cha kushangaza hakuna kauli inayosema lini tatizo hilo la mradi uliogharimu mamilioni ya pesa na nguvu za watu litashughulikiwa. Na hii imekuwa kawaida kwa miradi mingi Tanzania kukwama kutokana na kukosa uendelevu huku walioanziaha miradi hiyo wakisahau kuwa kiasi kikubwa cha pesa kimetumika kuanzisha miradi hiyo.
wananchi wakisubiri maji yatoke bila mafanikio
Moja ya bomba likiwa halitumiki kwa sasawananchi wakisubiri maji yatoke bila mafanikio