Mshambuliaji mpya wa klabu ya Everton ya nchini Uingereza Samuel Eto’o usiku wa kuamkia hii leo ametangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Cemaroon.Eto’o ametangaza hatua hiyo baada ya kuitumikia Cameroon kwa kipindi cha miaka 17 ambapo kwa muda wote huo ameweka rekodi ya kuwa mfungaji bora katika timu ya taifa baada ya kufungwa mabao 56.
Eto’o amewatakiwa kila la kheri wachezaji wenzake waliosalia kikosini na pia ameliombea dua njema taifa lake ili lifanikishe azma ya kufikia malengo Katika michuano itakayowakabili siku za hivi karibuni na miaka ijayo
"Kustaafu kwangu hakumaanishi nitakuwa mbali na timu ya taifa ya Cameroon, bali nitakuwa bega kwa bega na wachezaji watakaotajwa kila wakati, kwa ajili ya kuwapa morari na kuwahimiza wacheze kwa kujituma." Amesema Eto’o.
Mshambuliaji huyo ambaye aliwahi kuzitumikia klabu nguli barani Ulaya FC Barcelona, Inter Milan pamoja na Real Madrid alianza kuitumikia timu ya taifa ya Cameroon mwAaka 1997 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Costa Rica ambao walichomoza na ushindi wa mabao 5-0.
Na mchezo wake wa mwisho akiwa na timu ya taifa ya Cameroon ulikuwa dhidi ya Mexico wakati wa fainali za kombe la dunia zilizounguruma nchini Brazil mwaka 2014.
 
Top