Polisi waua raia St Louis nchi Marekani
Waombolezaji wakitoa heshima zao eneo ambalo Michael Brown aliuawa.
Kwa siku ya mpili mfululizo kumekua na mapambano katika mji wa Missouri nchini Marekani kufuatia kifo cha kijana mmoja mweusi ambaye alipigwa risasi na polisi katika kitongoji cha St Louis siku ya jumamosi.
Mkuu wa polisi wa kitongoji cha watu weusi cha Ferguson,Tom Jackson amesema kwamba polisi walitumia gesi na risasi za bandia ili kuwatawanya watu waliokua wamefurika karibu na jengo ambalo liliteketezwa kwa moto siku ya tukio ambapo maduka yaliporwa bidhaa na magari yaliharibiwa vibaya.
Ni wakati huo wa utumizi wa gesi na risasi bandia ndipo raia walipoamua kuwarushia mawe polisi,polisi nao wakajibu mapigo kwa kuwarushia risasi raia hao.
Kijana Michael Brown,alipigwa risasi kadhaa alipokua amening'inia kwenye gari ya polisi,na kufuatia tukio hilo FBI wanachunguza endapo kuna uvunjifu wa haki za binadamu katika tukio hilo la kuuawa kwa kijana Michael Brown.