Q-Chillah akionyesha Cd ya wimbo wake mpya uitwao 'Nipende Nikupende' aliofanya na MB Dog.
Q-Chillah akipozi na Wahariri wa Magazeti ya Global Publishers, Erick Evarist (kulia) na Siafel Paul (kushoto) baada ya mahojiano ya leo.
Q-Chillah akisalimiana na Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Michezo ya Championi, Saleh Ally.
Q-Chillah akiwa na Mhariri wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli.
Q-Chillah akifikiria jambo wakati akihojiwa na Global TV Online.
NGULI kwenye gemu la Bongo Fleva, Abubakar Katwila ‘Q-Chillah’ leo ametua katika studio za Global TV Online na kufanya mahojiano akifunguka kuhusu ujio wake mpya wa sasa. Staa huyo aliyesaini mkataba wa kufanya kazi na QS Mhonda J Company ameelezea mambo mengi kuhusu muziki wake na alivyojipanga kuwapa vitu vikali mashabiki wake.