Watu 16 wamefariki papo hapo baada ya Mabasi mawili waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso kwenye kijiji cha Morogoro wilayani Sikonge Mkoani TaboraTaarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Bi Suzan Kaganda amesema ajali hiyo iliyotokea jana Agosti 19,2014, majira ya saa 9 alasiri ambayo ilihusisha mabasi mawili ya Kampuni ya SABENA lililokuwa likitoka Mkoani Mbeya kwenda Mkoani Tabora pamoja na basi la AM Coach lililokuwa likitokea Mwanza kwenda wilayani Mpanda Mkoani Katavi.

Amesema waliotambuliwa ni 10 wakiwemo madereva wa magari hayo ambao ni Aristedis Shirima wa Basi la AM Coach na James Komba wa Basi la SABENA.

Mabasi hayo ya AM Coach na SABENA yamepata ajali ambapo chanzo cha ajali hiyo kimedaiwa kuwa ni mwendo kasi wa mabasi hayo,majeruhi wamelazwa kwenye hosptali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete ambao jumla yao ni 75,waliopoteza maisha jumla 17 na 10 wametambuliwa.

Aidha mmoja wa majeruhi aliyejitambulisha kwa jina la Christopher amesema ajali hiyo imesababishwa na vumbi kubwa lililotokea baada ya kupishana na gari jingine.

Kamanda Kaganda amewataka watu kwenda katika Hospitali ya wilaya ya Sikonge kwa ajili ya utambuzi wa marehemu waliobaki.




Baadhi ya Mashuhuda wa Ajali iliyohusisha mabasi mawili ya abiria kati ya SABENA ya Mbeya-Tabora na AM Dreamline ya Mwanza-Mpanda.


 
Top