Tetemeko la ardhi latikisa Afrika Kusini
Tetemeko la ardhi limetokea Afrika Kusini na kumuua mtu mmoja pamoja na kusababisha wachimba migodi kukwama katika machimbo Kusini Magharibi mwa Johannesburg.
Waokozi wanasema kuwa tetemeko hilo lilikuwa lenye vipimo vya 5.3 na lilitokea katika eneo la Orkney, kitovu cha machimbo ya dhahabu.
Inaariiwa watu katika nchi jirani za Botswana na Msumbiji waliweza kuhisi tetemeko hiloMtu mmoja alifariki baada ya ukuta katika eneo hilo la Orkney kuporomoka.
Maafisa wa uokozi walisema kwamba shughuli ya uokozi ilitakiwa kufanyika katika migodi inayozingira Orkney ingawa moja ya mgodi ulikuwa na tatizo.
Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg anasema kuwa eneo linalozingira mji huo, lina historia ya kukumbwa na mitetemo ya ardhi katika migodi ingawa yenye vipimo vya chini.
Migodi hiyo ya dhahabu ni ya kina kirefu
Wanajiolojia wametaja tetemeko hilo kama lenye kuonyesha dalili muhimu kwani lilitetemesha madirisha katika majengo marefu mjini Johannesburg.