Pande zote zinazohusika katika mgogoro wa Ukraine zinatumia makombora yaliyotengenezwa UrusiImedaiwa kuwa hakuna aliyenusurika katika shambulio la msafara wa wakimbizi katika mji wa Luhansk eneo lililo mashariki mwa Ukraine Jumatatu, taarifa ya waasi imeiambia BBC.
Taarifa za shambulio hilo bado hazijawekwa wazi lakini msemaji wa jeshi la Ukraine amesema miili ya watu 15 imepatikana kutokana eneo la tukio.
Ukraine imewashutumu waasi wanaoungwa mkono na Urusi kwa kuushambulia msafara wa wakimbizi lakini wamekana kuhusika na shambulio hilo.
Wakati huo huo, mapigano makali yameripotiwa katikati ya mji wa Luhansk.
Serikali ya Ukraine imesema Jumamne kuwa mapigano ya mtaani yalikuwa yakiendelea na afisa katika wizara ya mambo ya ndani ameliambia shirika la habari la Ukraine, Interfax kuwa jeshi limekuwa likikomboa mji "Kipande kwa kipande".
Zaidi ya watu 300,000 wamekimbia mapigano mashariki mwa Ukraine
Imeripotiwa kuwa katikati ya mji wa Luhansk kumekuwa na mashambulio ya risasi usiku wa Jumatatu.
Maelfu ya watu wameukimbia mji wa Luhansk, mmoja kati ya miji mikubwa miwili inayoshikiliwa na waasi wanaoungwa mkono na Urusi, wakati ambapo majeshi ya serikali ya Ukraine yanasonga mbele kuikomboa miji hiyo.
Mapigano pia yamekwamisha juhudi za kutafuta miili ya watu katika eneo la tukio kufuatia shambulio la Jumatatu usiku, katika barabara kati ya ya miji ya Novosvitlivka na Khryashchuvatye.
Zaidi ya watu 300,000 wamekimbia mapigano mashariki mwa Ukraine
chanzo:BBC