WANAFUNZI WAKALIA MADAWATI KWA ZAMU KUTOKANA NA UPUNGUFU ULIOPO
Hili ni darasa la saba ambalo nalo linawanafunzi zaidi ya 60 ambapo hupeana zamu kukaa kwenye madawati kutokana na upungufu uliopo wa madawati.
shule ya msingi Kano katika kijiji ch Amani halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Huyu ni mwenyekiti wa kijiji cha Amani Dotto Polepole akielezea changamoto mbalimbali katika shule hiyo na ukosefu wa madawati na kufanya wanafunzi kuendelea kukaa chini.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kano Shabani Masuma alisema katika kero zinazompasua kichwa ni ukosefu wa madawati na maji katika shule hiyo.
Hiki ni kikao cha serikali ya kijiji cha Amani kata ya Salawe halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ambapo hoja mbalimbali zilikuwa zikielezwa ikiwemo uchangiaji wa madawati kwa kila kaya ili kuweza kupata angalau madawati 30 kwaajili ya wanafunzi wa shule ya msingi Kano,ambapo mjumbe kwenye kamati hiyo Zoya Mstapha alisimama na kuchangia hoja kwenye kikao hicho.
WANAFUNZI wanaosoma katika shule ya msingi kano iliyopo kijiji cha Amani kata ya Salawe halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,wanalazimika kusoma kwa kupeana zamu kukaa kwenye madawati kutokana na shule hiyo kukabiliwa na upungufu mkubwa wa madawati na kusababisha usumbufu wakati wa kuandika.
Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kijiji hicho mwalimu mkuu wa shule hiyo Shabani Masuma alisema wanaupungufu mkubwa wa madawati ambapo yaliyopo ni 50 tu ambapo kuanzia darasa la pili hadi la sita wanakaa chini huku madara mawili la kwanza na la saba ndiyo wamepewa madawati hayo japo kuwa hayatoshi.
Mwalimu Masuma alisema kutokana na changamoto hiyo imekuwa ikisababisha wanafunzi kuwa na muandiko mbaya kwa kuwa hakuna sehemu nzuri ya kukaa ,huku akibainisha kwamba shule hiyo ina wanafunzi 536 kati yao wavulana ni 233 na wasichana ni 303 na kwamba darasa moja linawanafunzi zaidi ya 60.
“tunachangamoto ya uhaba wa madawati yaliyopo ni 50 na wanafunzi wako zaidi ya 500,wengi wao wanalazimika kukaa chini halafu wachache darasa la kwanza na la saba ndiyo wanakalia madawati ambayo pia hugombania kwa kuwa hayatoshi na kupeana zamu kukaa pia wastani wa wanafunzi 40 hawahudhurii vipindi kutokana na utoro”alisema mwalimu mkuu Masuma.
Mwalimu Magesa Masolele ni mmoja wa walimu wa shule hiyo alisema alisema miandiko ya wanafunzi hao inakatisha tamaa hata akiandika mwanafunzi wa darasa la tano, utafikiri ndio anaanza darasa la kwanza sababu ya kukaa chini hakuna mpangilio mzuri wa mwandiko hivyo inawapa shida walimu hasa katika usaishaji kwenye madaftari ndio maana wakaamuwa kupea na zamu kukalia madawati.
Naye mwenyekiti wa kijiji hicho Doto Polepole alisema kuwa changamoto ya uhaba wa madawati ni kubwa kwani hivi sasa serikali ya kijiji imeamua kuanza kupitisha michango kwa wazazi, ili kuweza kuchongesha madawati wanafunzi wapate unafuu wa kusoma na kuwaondoa kero hiyo.
Baadhi ya wazazi wa kijiji hicho John Mlewa na Samson Masasi walisema kuwa wazazi wanatoa michango mingi ya maendeleo na kuweka wazi kuwa suala la madawati halitafanikiwa kwa kupitia wazazi pekee kinachotakiwa ni serikali kuingilia kati suala hilo ili kuweza kuwakomboa wanafunzi kwani hata wao kama wazazi hawafurahishwi na hatua hiyo.
wataendelea kukaa chini mpaka lini hata wao kama wazazi hawafurahii hali hiyo.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo ambaye ni ofisa mipango Ambokisye Mwakabana alisema kuwa changamoto ya madawati ipo kwenye shule nyingi na zimetengwa fedha kwaajili ya kuchongesha madawati zaidi ya 500 na kutarajia kusambaza kwenye shule ambazo zinaupungufu mkubwa kwa kuzipatia madawati 30 kila shule ikiwa kuna shule 128 za msingi katika kata 26 za wilaya hiyo.