Licha ya kusitishwa vita, mapiganlo yaliripotiwa leo asubuhi
Serikali ya Israel imetangaza kuondoa wanajeshi wake wote katika maeneo wanakotekelezea mashambulizi nje ya ukanda wa Gaza.

Hatua hii inakuja saa chache baada ya makubaliano ya kusitisha vita kufikiwa. Makubaliano hayo yaliongozwa na wapatanishi wa Misri Jumatatu usiku.

Israel inadai kuwa lengo hasa la mzozo huo ni kuharibu mahandaki yanayotumiwa na wapiganaji wa Hamas na kwamba hilo limefikiwa.

Maafisa katika ukanda wa Gaza wanasema kuwa mgogoro huo wa wiki nne umesababisha vifo vya watu 1,800 katika eneo la wapalestina.

Idadi ya waisraeli waliofariki inakisiwa kua 67.

"Majeshi ya Israel,yatatakiwa kusalia katika maeneo ya ulinzi nje ya Ukanda wa Gaza hadi hali itakapotulia kabisa,'' alisema msemaji wa jeshi la Israel kanali Peter Lerner .

Dakika chache tu baada ya makubaliano ya kusitisha vita kufikiwa,mashambulizi ya angani yaliskika katika miji ya Jerusalem na Tel Aviv huku Hamas wakirusha makombora katika eneo la Kati mwa Israel.

Majeshi ya Israel pia yalishambulia Gaza muda mfupi baada ya makubaliano ya kusitisha vita kuanza kutekelezwa.
 
Top