WANAUME WAWILI WAFARIKI DUNIA KWA KUKOSA HEWA NDANI YA SHIMO WAKISAKA DHAHABU SHINYANGA
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha
Watu wawili(wanamme) wakazi wa kijiji na kata cha Mwakitolyo wilaya ya Shinyanga vijijini mkoani Shinyanga wamefariki dunia baada ya kukosa hewa wakiwa ndani ya shimo wakichimba mchanga uliodhaniwa kuwa na madini aina ya dhahabu.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari ya kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha tukio hilo limetokea jana majira ya saa tisa alasiri.
Amewataja wanamme hao kuwa ni Simba Mayeka(55) na Limwa Buguruti(35) wakazi wa kijiji cha Mwakitolyo.
Na Kadama Malunde-Malunde1 blog