MAMA mmoja (jina lake linahifadhiwa kwasasa) amefariki baada ya wahudumu wa zahanati moja ya mjini Iringa kujaribu kumtoa mimba bila mafanikio.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Jumatano ya wiki iliyopita katika zahanati hiyo iliyopo mjini hapa.
Baada ya taarifa hizo kuvuja, habari zilizoufikia mtandao huu zinaonesha kwamba Polisi walitia timu katika kituo hicho cha kutolea huduma jana na kuwakamata wahudumu wote waliokuwepo zamu katika Zahanati hiyo binafsi.
Wakati watoa huduma wakiachwa bila msaaada wowote katika selo ya Polisi Kati mjini Iringa,ndugu wa mkurugenzi huyo walifika na kumtoa mkurugenzi huyo baada ya kukamilisha taratibu za dhamana.
Mpashaji wetu amesema kabla ya kifo chake mama huyo alifika kituoni hapo akihisi ana ujauzito alioupata bila ridhaa yake.
Ili asitishe uhai wa kiumbe kilichoanza kuumbwa katika tumbo lake, mama huyo aliahidi kutoa sh 70,000 kwa mmoja wa watoa huduma wa zahanati hiyo ili atolewe mimba hiyo.
Kwa kuwa hakuwa na ujuzi, mtoa huduma huyo anadaiwa kutumia vifaa visivyotakiwa kutoa mimba hiyo hali iliyomsababishia mama huyo maumivu makali.
Hali ya mama huyo ilizidi kuwa mbaya baada ya kufika nyumbani kwake maeneo ya frelimo mjini Iringa.
Pamoja na ndugu wa mama huyo akiwemo mwanaume anayesadikika kuwa ni mumewe kumrudisha mama huyo katika zahanati hiyo, watoa huduma waliokuwepo zamu ya jioni ya siku hiyo aliyotolewa mimba, walihofia kumpokea kwa kile kinachoelezwa alikuwa katika hali mbaya.
Badala ya kumpeleka hospitali ya mkoa, ndugu hao walirudi na mama huyo nyumbani na taarifa zinaonesha kwamba alifariki saa moja baadaye.
Bada ya Polisi kunasa taarifa hizo walizuia mwili wa mama huyo usizikwe mpaka ulipofanyiwa uchunguzi na kubainika alikufa baada ya kukatwakatwa nyama za mlango wa uzazi wakati shughuli ya utoaji mimba ikiendelea.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi
anaendelea kutafutwa ili kuthibitisha taarufa hizi
Na Francis Godwin Blog