Ajali ya gari dogo imetokea jana majira ya saa 10 za jioni katika maeneo ya Tazara jijini Dar es salaam. Dereva wa gari hili (Toyota Landcruiser VX lenye namba za usajili T540 APN) aliruka mapema kabla ya tukio kutokea na alikuwa peke
yake.Kwa mujibu wa mashuhuda ni kwamba, dereva alipoteza muelekeo ktk kulikwepa gari aina ya fuso lililokuwa kando ya barabara.Hakuna aliyepoteza maisha katika ajali hiyo.