Licha ya kuwepo kwa vitisho vinavyowataka wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutoingia bungeni, Bunge hilo limeendelea chini ya ulinzi mkali wa jeshi la Polisi huku barabara kuu ya kuingia na kutoka mjini Dodoma inayokatiza mbele ya jengo hilo ikiwa imefungwa .
Wakati ulinzi huo ukiendelea kamati 12 za Bunge hilo zilikuwa zikiwasilisha mapendekezo ya mambo ambavyo wangependa yawepo katika rasimu ya katiba inapopendekezwa.
Kwa upande wa kamati namba mbili imependekeza kuwa rasimuhiyo ya katiba itamke wazi kuwa watu wenye ulemavu hawatabanguliwa ili kukomesha tabia ya baadhi ya watu kuwabagua wenye ulemavu.
Aidha kamati namba saba imependekeza kutungwa kwa sheria ya kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya rushwa na uhujumu uchumi ambapo sheria hiyo ibainishe majukumu ya moja kwa moja kwa taasisi ya kuzuia rushwa.
Katika hatua nyingine mwanasheria mkuu wa serikali Jaji Fredrick Werema ametoa ufafanuzi bungeni kuhusu maamuzi yaliyotolewa na mahakama kuu kuhusu kesi iliyokuwa imefunguliwa na Saidi Kubenea.