Umoja wa wana Ngara waishio Dar Es Salaam wamepata rasimu ya kwanza ya katiba ambayo itajadiliwa ili kupendekezwa kuwa katiba kamili ya umoja huo. Hayo yamejiri katika mkutano wa umoja huo uliofanyika jana tarehe 27/09/2014 katika ukumbi wa KALEMBO HOTEL Buguruni jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti msaidizi wa umoja huo ndugu John Meshack akiwasilisha rasimu ya katiba mbele ya wajumbe.
Wajumbe wakifatilia kwa makini uwasilishwaji wa katiba hiyo.
Wajumbe wakipitia vipengele vya katiba ili kubaini mapungufu na kutoa maoni ya kipi kiongezwe na kipi kipunguzwe.
Baadhi wa wajumbe waliochangia kwenye uboreshwaji wa rasimu ya katiba hiyo ya wanangara waliipongeza kamati ya bwana Asheri Majanja iliyokusanya maoni kwa wanangara waishio Dar es salaam na hatimaye kupelekea kupatikana kwa rasmu hiyo yenye vipengele muhimu kama madhumuni ya umoja, sifa za mwana umoja, miradi ya maendeleo ya umoja, maendeleo ya miradi ya wilaya ya Ngara, muundo wa uongozi, adhabu za kukiuka katiba na vyanzo vya mapato ya umoja huo.
Mmoja wa wanangara ndugu Abel Ngwebe alichangia sura ya 13 inayotaja miradi ya maendeleo kwa kupendekeza kuingizwa kifungu kitakachompa mamlaka mwenyekiti kuunda kamati itakayoratibu na kukusanya taarifa ya hali ya maendeleo ya wilaya ya Ngara ili kujua ni maeneo yapi ya wilaya ya Ngara yatapewa kipaumbele kwenye miradi hiyo.
Wakichangia kifungu cha sifa za mwanachama baadhi ya wajumbe walipendekeza wanangara wanaoishi mikoa jirani mf. Morogoro na Pwani wawe na sifa ya kuwa wanaumoja huo.
Mzee Timoth Kaholo mzaliwa wa Kashinga Nyakisasa ambaye ni mwana umoja wa wanangara.
Mjumbe akichangia hoja