Moto uliowaka zaidi ya saa 9 umeteketeza meza zaidi ya 250 na maduka zaidi ya 330 ya wafanyabiashana huku Wananchi wakihangaika kuuzima kwa kutumia mchanga katika soko kuu la mji mdogo wa Urambo mkoni Tabora usiki wa kuamkia October 13,2014, katika kile kilichohisiwa kuwa unaweza kuwa umesababishwa na mamalishe ndani ya soko.
Wakiongea kwa masikitiko baadhi ya wafanyabiashara walioathiriwa na moto huo, katika soko hilo wameiomba serikali kujitahidi kuwaondoa akina mama lishe na mafundi wa kushona nguo kuwaondoa katikati ya maduna na meza kwani inawezekana kuwa, waliacha moto ukiwaka na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha ambayo haikupatikana mara moja.
Aidha akizungumzia changamoto iliyowakumba Wananchi wa kata hiyo kutokana na Kupoteza Mali zao kulikosababishwa na kuungua kwa soko hilo, Diwani wa kata ya Urambo mjini Bw. Amatus Liumba ameomba Wananchi kujenga tabia ya uaminifu kwani katika kuokoa mali nyingi zilihamia katika njia za panya na kutoweka.
Juhudi za kumpata Afisa Biashara Wilaya ya Urambo, Bw. Hatibu Abdulahamani ili kujua kiasi gani cha hasara walichokipa Wafanyabishara hao zinaendelea kutokana na tathimini zinazoendelea kufanyika.
Habari/Picha Na:-Mwanawamakonda