Watu wawili namenusulika kifo baada ya kontena la kunde kudondoka kutoka juu ya gari la mizigo lililokuwa kwenye mwendo kasi, likitokea Mbagala rangi tatu likielekea Kariakoo jijini dar es salaam.
Taarifa zinasema kwamba hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa katika tukio hilo, isipokuwa vijana wanaoishi maeneo hayo walianza kuzoa Kunde baada ya kontena kuanguka kabla ya polisi kufika.
Imeelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo nikutofungwa vizuri kwa kontena hilo pamoja na bodi la gari la mizigo husika na kwamba Ajali hii imetokea leo Octob 05,2014 katika Eneo la Msikitini kati ya Mtongani na Mission jijini Dar es Salaam.Picha Na:-Mutalemwa Blog.