Mwenyekiti wa BAWACHA ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kawe kupitia CHADEMA –Bi.Halima Mdee akiwa katika maandamano, akiwaongoza Wanawake wenzake kuelekea Ikulu kwa lengo la kumshinikiza Rais Jakaya Mrisho Kikwete kutosaini Rasimu ya tatu ya katiba iliyopendekezwa Bungeni Octoba 02,2014 mjini Dodoma, maandamano hayo kabla hayajafika mbali yalitawanywa na Jeshi la Polisi lililotumia maji ya kuwasha pamoja na kupigwa kwa waandamanaji na kumshika Mwenyekiti huyo Halima Mdee pamoja na wafuasi wake na kupelekwa Kituo cha Polisi Osterbay jana Octoba 04,2014.


Askari Polisi wakimpandisha Halima Mdee kwenye gari la Polisi baada ya kumkamata hapo jana Octoba 04,2014 na Wananchama wenzake wa CHADEMA.


Mfuasi wa CHADEMA akishikiliwa na Polisi na kupelekwa katika gari la Polisi ambapo Katika kudhibiti maandamano hayo jeshi la polisi walitumia maji ya washawasha kutawanya wafuasi hao wa CHADEMA.


Ni katika mtaa wa Togo Kinondoni jijini Dar es salaam na ni muonekano wa baadhi ya wafuasi wa Chadema kutoka Baraza la wanawake wakiwa katika ofisi tayari kujiandaa na maandamano hayo ambapo Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa,Halima Mdee akizungumza na vyombo vya habari akasema maandamano ni haki,na katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania inaruhusu watu kuandamana.


Halima Mdee akiwa ndani ya gari la polisi pamoja na wafuasi wa chadema wakipelekwa katika kituo cha Polisi cha Osterbay.


Mwenyekiti wa Bawacha taifa Halima Mdee akizozana na Polisi mara baada ya kuingizwa kwenye gari.




Viongozi wa CHADEMA wakiomba kuruhusiwa kupita Polisi ya Osterbay ambapo Katibu mkuu wa CHADEMA, Mh Wilbrod Silaa akizungumza na ITV kwa njia ya simu na kusema kuwa tayari wanasheria wa chama chao wanalishughulikia sakata hilo.


Picha juu na chini ni Wafuasi wa CHADEMA wakimueleza Askari Polisi madai yao wakiwa nje ya kituo cha Polisi cha Osterbay wakidai kwenda kwa wanaohusika kutuoni hapo kwa ajili ya kumtoa Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa, Halima Mndee.


 
Top