Ligi soka wilaya ya Ngara mkoani Kagera yenye lengo ya kupata Bingwa wa wilaya 2014/2015,imeendelea tena leo October 12,2014 katika viwanja viatu tofauti ambapo Uwanja wa kokoto mjini Ngara ,Timu ya Walimu FC imefanikiwa kuungana na Kabanga FC hatua ya robo fainali kutoka kundi A baada ya kuifunga kwa binde Mabawe FC bao 1-0. 
Katika uwanja wa Rulenge timu ya Ngara Stars imeiadhibu timu ya Nyakisasa FC kwa jumla ya goli 3-0 na hivyo kuungana na Rulenge White Stars hatua ya robo fainali kutoka kundi lao la C.

Katika uwanja wa Benaco,Timu ya Rusumo FC ilizinduka baada ya kuchapwa bao 1-0 na Ngara Boys FC na kuiadhibu Benaco Stars bao 2-1. 

Katika kundi hili la B,Timu zote Benaco Stars ,Rusumo na Ngara Stars zimemaliza michezo yao kwa kulingana Pointi 3 na goli Moja moja.
 
Top