Pichani ni Kabanga fc wakichuana na Mabawe fc uwanja wa kokoto
Ligi ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera imeendelea leo katika viwanja tofauti vilivyopangwa kuchezewa mechi hizo. Katika uwanja wa Rulenge timu ya Rulenge white stars imeiadhibu timu ya Nyakisasa kwa jumla ya gori 9 kwa 1.
Katika uwanja wa Benaco timu ya Ngara boys imeilaza timu ya Rusumo fc kwa gori 1 kwa 0. Na katika uwanja wa kokoto mjini Ngara, timu ya Kabanga Fc imeilaza timu ya Mabawe fc kwa gori 3 kwa 2 na hivyo timu ya Kabanga fc imejihakikishia kuendelea na michuano ya ligi hiyo. Pia timu ya Rulenge white stars imejihakikishia kuendelea na michuano baada ya kupata point tatu zilizoifanya ifikishe point 4 maana mechi yao ya kwanza waliondoka na point moja.