Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee na wenzake tisa wamepelekwa katika Gereza la Segerea jijini Dar baada ya kushindwa kutimiza baadhi ya masharti ya dhamana yao.
Mdee na wenzake nane mapema leo walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar na kukana tuhuma zinazowakabili.
Mdee na wenzake hao wanashitakiwa kwa makosa mawili kototii amri za maofisa wa polisi na kufanya maandamano kinyume na sheria Jumamosi iliyopita ya Oktoba 4, mwaka huu.
Watapandishwa tena kizimbani hapo kesho Octoba 08,2014,saa 4 asubuhi.
(Habari na Deogratius Mongela/GPL)