Habari za Siku ndugu,
Nina imani wengi wenu mna hamu ya kupata uhalisia wa habari zilizoeneamitaani kuhusu mwanafunzi kumzalisha mwalimu wake katika shule ya Nkasi ambayo ndiyo kituo changu cha kazi.
Nitafafanua kwanza kuhusu walimu wa kike ninaofundisha nao then ntafafanua mazingira ya kuandikwa hiyo habari ilivokuwa.
Kwanza shule ya sekondari ya Nkasi ipo wilayani Nkasi mkoa wa Rukwa. Shule hii ina kidato cha 1 hadi cha 6 ikiwa na tahasusi za HGK, HGL, PCM na PCM (wasichana na wavulana). shule ina walimu 5 wa kike kama ifuatavyo:
Madam Kasanga, huyu ni mama wa makamo amehamia mwezi uliopita kutoka morogoro, ana watoto wakubwa na mme wake ni askari magereza.
Madam Mwamini, huyu ni mdada mdogo tu, ana mtoto mdogo ananyonyesha ni mke halali wa mtu na anaishi na mmewe, mme wake anafanya kaz LAPF.
Madam David, huyu ni mdada tumeripoti nae mwaka huu. Hana mtoto ila ni mke halali wa mtu, mmewe ni mwalimu anafundisha Sumbawanga manispaa.
Madam ipungu, huyu ni msichana hana mtoto ila mpaka sasa nina kadi yake anatarajia kufunga ndoa mwez wa 12.
Madam Balama, huyu pia ni mdada na hana mtoto.
Pili, mazingira ya hiyo habari kuandikwa ni kutokana na taasisi inayoitwa TMEP (Tanznia Men Equal Partinership) taasisi hii inajihusisha na elimu ya kuwahusisha wanaume katika maswala ya afya ya uzazi na malezi. Taasisi hii inafanya kazi kwenye mikoa 2 tu yaani Rukwa na Singida.
Tar 1/10/2014 taasisi hii ilitembelea shuleni kwetu kama wakala kuja kukagua maendeleo, viongozi hao wakiwa wameambatana na mwandishi wa habari (Siame) alimuuliza mkuu wa shule (Mr. Manga) je! kuna umuhimu wa hii elimu kutolewa ? Mkuu katika kujibu swali hilo akamwambia kuna umuhimu sana kwani siku za nyuma katika shule ya msingi kabwe iliyopo katika mwambao wa ziwa mwalimu wa shule ya msingi alizalishwa na kijana wa kidato cha pili hii yote ikiwa ni kwasababu ya kijana kukosa elimu ya malezi.
Lakini tangu elimu hii imeanza kutolewa tumeona mimba za ovyo ovyo kwa vijana zimepungua pia ushiriki wa wanaume kwenye masuala ya malezi ya watoto umeongezeka.
Sasa tatizo la waandishi makanjanja akaripoti kama ndio tukio jipya na limetokea Nkasi akiongeza na ubunifu wa maneno ili habari yake ishike kurasa za mbele za vyombo vya habari.
Kimsingi hakuna ukweli wowote na sisi tukiwa kama taasisi tunafikiria kuchukua hatua za kisheria kwa kuharibiwa Taswira yetu katika jamii.
Ukweli ndio huo ndugu zangu.
Ahsanteni.
Mwl Mwaipaja. M. l (akabhofu!!!!)
Nkasi High School
P.o Box 119
Namanyere- Nkasi