Wazazi wameshauriwa kuwakataza vijana wao waliohitimu darasa la saba kujiepusha na biashara ya bodaboda na badala yake waendelezwe kimasomo ili wafanikiwe kupata elimu ya juu.
Ushauri huo ulitolewa na Mkuu wa Shughuli za Benki ya Wanawake Tanzania, Zabron Yebete jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Yebete alisema vijana wengi wamekuwa wakihitimu darasa la saba na kukimbilia kufanya biashara ya bodaboda badala ya kufikiria kujiendeleza na masomo.
Aliyasema hayo wakati wa mahafali ya Shule ya Msingi Kifulu iliyoko katika Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.