Miss World Tanzania, Happiness Watimwanywa akiwa London
Mshiriki anayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss World, Happiness Watimanywa amewashukuru watanzania kwa kuanza kuonesha muamko wa aina yake na kumpigia kura kuiwezesha Tanzania kuingia katika orodha ya 10 bora ya Chaguo la Watu la washiriki wenye nafasi ya kushinda Miss World Mwaka huu.
Mrembo huyu ameweza kuongea na EATV kupitia show kali ya Friday night Live akiwa jijini London na kusema kuwa, sapoti ya watanzania imemuongezea nguvu na atasimama akijua kuwa anaiwakilisha nchi na si yeye binafsi.
Zoezi la kumuwezesha mshiriki huyu kufanya vizuri katika orodha hii, linaendelea mpaka siku ya Jumapili kwa njia ya kumpigia kura mtandaoni kwa kupitia 'application' maalum iliyotengenezwa na Miss World .
Mfumo huo unakupatia nafasi ambapo unapata fursa ya kuchagua washiriki watatu wa mashindano hayo unaowakubali zaidi zikiwa zimebaki siku mbili tu kuelekea fainali ya mashindano hayo.