Idara ya Uhamiaji nchini imesema asilimia kubwa ya matatizo yanayoikabili ni pamoja na mchakato wa utoaji wa hati za kusafiria na tatizo la wahamiaji haramu ,yanatokana na uelewa mdogo wa wananchi juu ya majukumu ya idara hiyo na ugumu unaojitokeza katika utekelezaji.
Akizungumza katika mkutano wa mwaka wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa idara hiyo unaofanyika Jijini Arusha , Kaimu Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Bw ana Peniel Mgonja amesema,kwa asilimia kubwa , matatizo hayo yanatokana na utamaduni wa wananchi wengi , kutaka kupata huduma kwa njia za mkato na pia kutumia muda mwingi kulalamikia mambo ambayo utatuzi wake uko ndani ya uwezo wao.
Kuhusu tatizo la wahamiaji haramu, Bwana Mgonja amesema pamoja na kuchangiwa na kuwepo kwa njia nyingi za panya katika mpaka wa Tanzania na majirani zake , pia linachangiwa na baadhi ya wananchi kurubuniwa na kujikuta wakiwasaidia wahalifu.
Akifungua mkutano huo , Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bwana Mbarak Abdulwakili amewataka wateandaji kujenga utamaduni wa kuwaeleza wananchi ukweli kwa mambo yanayowezekana na yasiyo wezekana ili wasipoteze muda n a kwa yale yaliyoko nje ya uwezo wao wayafikishe mapema panapohusika .