Mwaka mmoja baada ya vita kuanza tena Nchini Sudan Kusini, Katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Banki Moon anasema uhasama uliopo kati ya mahasimu wakuu wawili wa taifa hilo ndio unaotumbukiza taifa hilo katika lindi la uhasama.
Bwana Ban anawashutumu vinara hao Salva Kirr na Riek Machar kwa kukubali tamaa zao kuyumbisha hali tete ya usalama katika taifa hilo changa.
Ban Ki-moon anasema kwamba kushindwa kuafikia mapatano unahatarisha maisha ya mamilioni ya watu, na nia kuu ya shughuli za upaganiaji wa uhuru wa taifa hilo, kukosa maana.
Mapigano kati ya makundi hasimu tiifu kwa Rais Salva Kiir na yale yanayomuunga mkono makamu wa zamani wa Rais Riek Machar, yamesambaratisha kabisa miji mikuu muhimu Nchini humo.
Maelfu ya watu wamefariki katika mzozo huo huku mamilioni wakislaia kutegemea misaada ya kibinadamu.
CREDIT: BBC