Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania

Nchini Tanzania, zoezi la kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo mpya unaojulikana kama Biometric Voter Registration - BVR limekuwa likeendelea. BVR ni mfumo wa utambuzi wa wapigakura wengi na kwa haraka kwa kutumia alama za kibailojia kama vidole, macho au sauti.
Lengo la zoezi hili ni kuhakikisha utumiaji wa daftari hilo jipya kwa ajili ya kura ya maoni na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini humo mwakani. Hivi karibuni makamu mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi Jaji Mkuu mstaafu Zanzibar Hamid Mahamoud Hamid alikutana na viongozi wa vyama vya siasa nchini kuwapa taarifa kuhusu kuanza kwa shughuli za uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.

Tume imechukua hatua hiyo ili kuondokana au kupunguza utata katika uchaguzi ambapo kwa mfumo wa kidigitali utadhibiti udanganyifu kwa wapiga kura. Mpaka sasa tume ya taifa ya uchaguzi inaendelea kutoa mafunzo kwa watendaji wa tume,ambao ndiyo watakuwa wakufunzi. Mashine ya BVR inauwezo wa kuandikisha watu Zaidi ya 50 kwa saa.

 
Top