Mamia ya wananchi wa Afrika Kusini, maveterani wa vita vya ukombozi, maofisa wa serikali, na wanafamilia wa Hayati Nelson Mandela wamekusanyika katika ofisi za serikali zilizoko Pretoria, Afrika Kusini, katika hafla ya kuweka mashada ya maua ikiwa ni kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha Mandela.
Familia ya Mandela ikiongozwa na mkewe Graca Machel na Mandla Mandela, waliweka mashada ya kwanza kwenye sanamu kubwa ya Mandela iliyo nje ya ofisi hizo. 

Akizungumza kwa niaba ya familia, Graca ameitaka dunia na Afrika Kusini kuendeleza urithi aliouacha Hayati Mandela kwa njia yoyote inayowezekana. Amewataka raia wa Afrika Kusini kumheshimu Mandela kwa kupambana na changamoto za rangi, ukosefu wa usawa, umasikini, na ukosefu wa ajira. 

Mandela alifariki Disemba 5 mwaka jana mjini Pretoria, Afrika Kusini.

 
Top