Kocha Marcio Maximo ameendelea na mazoezi ya kuinoa Yanga.
Kocha huyo amefanya hivyo jana na leo ikiwa ni sehemu ya kuonyesha hatambui suala la kuondolewa kwake kazini.
Ingawa tayari alishafanya mazungumzo na uongozi wa Yanga kuhusiana na hilo, taarifa zinaeleza bado hajakabidhiwa barua rasmi.
Kocha huyo Mbrazil na msaidizi wake, Leonardo Neiva waliendelea na kazi yao kama kawaida kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola.
Tayari Kocha wa zamani wa Yanga, Hans van der Pluijm raia wa Uholanzi yuko jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Mbrazil huyo.