Muda wowote kuanzia sasa Rais Jakaya Kikwete atatoa na kutangaza uamuzi wake kuhusiana na baadhi ya watendaji wakiwemo Mawaziri kuhusishwa katika kashfa ya wizi wa fedha za Tegeta Escrow.
Wiki iliyopita Rais alipokea na kupiia ripoti iliyowasilishwa kwake,nyaraka na ushauri uliotolewa katika maazimio ya Bunge kuhusu akaunti ya Tegeta Escrow.
Kikwete ambaye alianza kazi Desemba 8 mwaka huu baada ya mapumziko kutokana na kufanyiwa upasuaji alisema atatoa uamuzi wake ndani ya wiki hii.
Alisema atatolea maamuzi mambo ambayo yanamuhusu yeye moja kwa moja na yale yanayohusu Serikali atatolea uamuzi na maelekezo ya namna ya kuyashughulikia.
Bunge lilitoa maazimio mbalimbali kwa Serikali ikiwemo kuitaka mamlaka ya uteuzi kuwawajibisha ikiwani pamoja na kuwavua nyadhifa zao Waziri wa Nishatina Madini,Mwanasheria mkuu,Waziri wa nyumba na maendeleo ya makazi,Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na madini na wengineo.
Chanzo Gazeti la Uhuru