Wakati zoezi la kupiga kura uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa kwa ngazi za vijiji, vitongoji pamoja na mitaa ukiendelea leo nchi nzima hali si shari mkoani simiyu katika wilaya ya Busega.
Taarifa zilizotolewa na jeshi polisi Mkoani Simiyu pamoja na Mkuu wa Wilaya hiyo Paul Mzindakaya zinaeleza kuwa katika mji wa lamadi viongozi walikuwa wanagombea katika uchaguzi huo kupitia CCM wamejiondoa katika dakika za mwisho.
Taarifa hizo zilieleza kuwa viongozi hao wamejiondoa kwa madai ya kutishiwa kuuawa, kuchomwa moto nyumba zao ikiwa pamoja na familia zao kuuawa na wafuasi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.
Majira ya asubuhi, kamera yetu katika pita pita kukagua hali ya upigaji kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa. Mkoani Simiyu mamia wajitokeza kupiga kura, vituo vimefunguliwa ndani ya muda lakini ni baadhi. katika wilaya ya Itilima mpaka muda huu baadhi ya maeneo vituo bado havijafunguliwa kutokana na masanduku ya kuchelewa.
Usalama kama kawaida ni wakutosha.
Walemavu nao kama kawaida wakipewa kipaumble.
Wakati zoezi la kupiga kura uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa kwa ngazi za vijiji, vitongoji pamoja na mitaa ukiendelea leo nchi nzima hali si shari mkoani simiyu katika wilaya ya Busega.
Taarifa zilizotolewa na jeshi polisi Mkoani hapa pamoja na Mkuu wa Wilaya hiyo Paul Mzindakaya zinaeleza kuwa katika mji wa lamadi viongozi walikuwa wanagombea katika uchaguzi huo kupitia CCM wamejiondoa katika dakika za mwisho.
Taarifa hizo zilieleza kuwa viongozi hao wamejiondoa kwa madai ya kutishiwa kuuwa, kuchomwa moto nyumba zao ikiwa pamoja na familia zao kuuawa na wafuasi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.
Mzindakaya ameeleza kuwa katika uchaguzi huo katika kijiji cha Lamadi, wagombea wa kutoka CHADEMA walienguliwa kutokana na kutokidhi vigezo baada ya kuwekewa pingamizi na CCM.
Alisema kuwa baada ya CHADEMA kuenguliwa walibaki wagombea kutoka CCM, huku akieleza kuwa mpaka jana jioni ofisi yake ilikuwa na taarifa za kuwepo chama kimoja kinachotakiwa kupigiwa kura.
Alibainisha kuwa hata hivyo leo (jana) asubuhi walipokea taarifa kutoka Mgombea nafasi ya Mwenyekiti wa Kijiji kupitia CCM aliyejulikana kwa jina moja Vumi pamoja na wajumbe wake kujitoa katika kinyanganyilo hicho kutokana na kutishiwa maisha yao.
“…mpaka sasa majira ya saa sita mchana…tumeamua kusitisha zoezi la kupiga kura..masanduku yote tumeyaondoa…na hali siyo swali katika eneo hilo…askari wamepelekwa kuweka hali ya usalama…na kamati ya ulinzi na usalama wilaya muda huu itaakaa kuweza kujadili hali hii..ili tukubaliane kama tuendelee na zoezi au tusitishe” Alisema Mzindakaya.
Kwa upande wake Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani hapa Charles Mkubo alisema kuwa jeshi lake limejiandaa kukabiliana na hali ya vurugu itakayojitokeza katika mji huo wa lamadi.
“….Taarifa hizo ni kweli pale lamadi watu hawajapiga kura kutokana na wagombea wa CCM kujitoa dakika za mwisho baada ya kutishiwa maisha yao na wafuasi wa chadema…na sisi jeshi la polisi tumeimarisha usalama hapo”
Kamanda Mkumbo ameongeza kuwa kwa mkoa mzima wa Simiyu hali ni shwari kiusalama huku afafanua kuwa baadhi ya maeneo kulikuwepo na kasoro ndogondogo za kucheleweshwa masanduku ya kupigia kura.