Watu wawili wamefariki papo hapo baada ya lori la mizigo aina ya fuso,kuiparamia pikipiki ya magurudumu matatu maarufu kwa jina la bajaji katika barabara kuu itokayo singida mjini kuelekea mwanza.
Akielezea tukio hilo kamanda wa polisi mkoani singida ACP Thobias Sedoyeka amesema tukio hilo limetoka siku ya tarehe mbili saa moja na dakika hamsini usiku ,baada ya dereva wa gari la mistubishi fuso yenye usajili wa namba T.641 AVH ambaye alikuwa amelewa kuanza kuparamia magari mawili kwa nyakati tofauti na baadaye kuigonga bajaji ambayo ilikuwa na abiria moja na dereva na kusababisha vifo vya watu wawili papo hapo.
Akithibitisha kutokea kwa vifo hivyo kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa singida Daktari Daniel Tarimo ,amesema wamepokea miili ya watu wawili moja ametambulika kwa jina la Thadei Antony Maleo ambaye alikuwa dereva wa bajaji na mwili wa mwanamke ambaye haja fahamika kwa jina anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya ishirini na tano na thelasini.
Kwa upande wao mashuhuda wa ajali hiyo pamoja na kueleza kuwa dereva wa fuso alikuwa akiendesha gari kwa mwendo wa kasi bila ya kuwa na tahadhari ,wameshauri madereva kuacha kutumia vileo pindi wanapokuwa katika kazi zao za kuendesha magari, kwani wamekuwa wakisababisha vifoo na hasara kwa uzembe.
Katika kipindi hiki cha mwishoni mwa mwaka pamoja na kusherehekea sikuku ambazo zina kuja,kila mwaka kumekuwa na matukio ya ajali mbalimbali kutokana na uzembe wa madereva ,jambo ambalo lina changia kupoteza maisha ya watu wasio kuwa na hatia na kuwasababishia ulemavu.
CHANZO: ITV TANZANIA