Mtu mmoja ambaye hakuweza kufahamika mara moja amegongwa na TRENI katika eneo la Kingolwira nje kidogo ya mji wa Morogoro na viungo vya mwili kusambaa zaidi ya mita mia moja. Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia askari na wananchi wakiokota vipande vya viungo vya mwili ikiwemo miguu na mikono na hawakufanikiwa kukipata kichwa ingawa viungo vingine kama miguu mikono kifua vilipatikana.

Wananchi wa eneo la Kingolwira wamesema huenda mtu huyo alikuwa mlevi alikuwa anavuka reli usiku bila kuchukua tahadhari

Station master mkoa wa Morogoro Flavian Nyawale amesema wamekabidhi jeshi la polisi tukio hilo ili kufanya uchunguzi na kutoa tahadhari kwa wananchi watembea kwa miguu kuach akutembea kando kando ya reli na kuchukua tahadhari wakati w akuvuka katika makutano ya reli na barabara ili kuepusha matukio ya ajali zisizo za lazima.

Kamanda wa reli Enginea Simon Chillery akizungumza kwa njia ya simu akiwa njiani kuelekea nachingwea amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema mtu huyo ambaye hakufahamika jina lake anakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 35 na 40 na uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na kuwakumbusha wananchi kuheshimu sheria za reli kama ilivyo sheria za barabarani kwa watembea kwa miguu na wanaendesha vyombo vya moto wanapovuka reli.
Source:ITV
 
Top