WAKATI Watanzania wakisubiri hatima ya Waziri wa Madini na Nishati Profesa Sospeter Muhongo, ambaye Rais Kikwete alisema anamuweka kiporo kutokana na kashfa ya Escrow, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mh Andrew Chenge, ametangaza rasmi kuachia nafasi hiyo.
Bunge lililopita baada ya kujadili ripoti CAG kuhusu miamala ilyofanyika kwenye akaunti ya Tegeta Escrowiliyokuwa imefunguliwa Benki Kuu ya Tanzania, lilipitisha maazimio manane ikiwemo kuwajibishwa viongozi wa Serikali na wale wa kamati za Bunge walionekana kuhusika katika kashfa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa, Chenge alitangaza kujiuzulu nafasi yake juzi baada ya kamati yake kukutana kwenye ofisi ndogo za Bunge jijijni Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya shughuli za Bunge, John Joel, alipotakiwa kuthibitisha hili, alisema hayuko ofisini, hivyo hawezi kuwa na jibu la moja kwa moja.
Chanzo:-Cloudsfm Radio