Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara Bw John Nshimilimana (Pichani mwenye miwani) akitazama ramani inayoonesha taswira ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera hivi karibuni akiwa na Madiwani wenzake wakati wa ziara ya kukagua Maendeleo wilayani Ngara. Halmashauri ya wilaya ya Ngara Mkoani Kagera huenda ikasimamisha shughuli zake za maendeleo, kutokana na uhaba wa fedha za maendeleo zinazotegemea ruzuku kutoka serikalini na vyanzo vyake vya mapato.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara Bw John Nshimilimana, amesema hayo wakati akiongea na RADIO KWIZERA FM, ambapo amesema kuwa kutokana na uhaba huo wameshindwa kufanya vikao halali kutokana na ukosefu wa posho.
Bw Nshimilimana amesema uhaba huo ulianza mwezi Octoba mwaka jana,2014 ambapo Halmashauri hiyo ilitegemea kupokea fedha za ruzuku Shilingi bilioni 2.5 lakini hadi sasa haijapokea fedha hizo hali inayosababisha miradi ya maendeleo kusimama.
Amesema baadhi ya miradi iliyokosa fedha na kusimama ni pamoja na maji, ukarabati wa barabara za vijiji wilayani humo, huku idara ya afya ikishindwa kufika katika vituo vya kutolea huduma kwa kukosa mafuta ya kusafiria.
Chanzo:-Radio Kwizera/Habari.