Jeshi nchini Chad linaendelea kufanya mashambulizi dhidi ya wanamgambo wa Boko Haram eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Ripoti zinasema kuwa ndege zake zilindesha mashambulizi kwenye mji wa Gamboru karibu na mpaka na Cameroon.
Siku ya Ijumaa Televisheni nchini Chad iliripoti kuwa jeshi la nchi hiyo liliwaua zaidi ya wanamgambo 120.
Waandishi wa habari wanasema kuwa kumekuwa na ushirikiano kwenye vita dhidi ya Boko Haram licha ya utawala nchini Nigeria kukosa kukiri kuwa wanajeshi wa Chad wamefanikiwa.